GAZETI LA UCHAMBUZI MAKINI LENYE KUIHUSU NA KUIGUSA JAMII. NI GAZETI LA KILA WIKI. LITAANZA KUONEKANA MITAANI JUMANNE, MACHI 31, 2009. USIKOSE NAKALA YAKO!
Sunday, December 06, 2009
Mjadala Uliobadili Mwelekeo; Ni Mrefu Kushinda Yote, Una Miaka Miwili Na Bado Uko Laivu!

( Pichani Ni JK Na Mwandosya, enzi hizoo). Mjadala huu ulianza Septemba, 2007, unaendelea hadi hii leo!)

# 25 November 2009 at 11:21 pm
Miaka Ile said:
Wametajwa hapa viongozi kutoka wilaya ya Rungwe ambao pia walikuwa miongoni mwa viongozi wa taifa letu; kati yao, akina Jeremiah Kasambala, David Mwakyusa na Mark Mwandosya ambao wote walikuwa ni mawaziri. Wawili, Mwakyusa na Mwandosya, bado ni mawaziri ninapoandika haya.

Lakini tusiwasahau mawaziri wengine kutoka wilaya hiyo ya Rungwe. Kabla ya kugawanywa katika wilaya mbili, Rungwe na Kyela, kulikuwa na kiongozi mwingine kutoka wilaya hiyo ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza wa nchi yetu ilipopata uhuru. Ingawa hakuwa waziri mwanzoni, alipewa uwaziri baadaye. Kiongozi huyo ni Julie Manning, kutoka Kyela,...Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
 
©Maggid | Date:6.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Saturday, December 05, 2009
Wapi Hapa? Jibu Ni ...


Kona ya Morogoro Road na Jamhuri Street
 
©Maggid | Date:5.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 8
Friday, December 04, 2009
Kilimanjaro Stars Kupalilia au Kuunguza Kibarua cha Maximo Leo
4/Deemba/2009
Kilimanjaro Stars inajitupa kuwania pointi tatu muhimu za kuiwezesha kusonga mbele katika fainali zakuwania kombe la Challenge dhidi ya Burundi ambayo imekwisha tolewa. Mchezo huo utakaopigwa majira ya saa nane alasiri unategemewa kuwa na kila aina ya ushindani kutokana na ukweli kwamba Burundi itakuwa na nia ya kulinda heshima yake ya kushinda walau mchezo mmoja.

Kocha wa Kilimajaro Stars Marcio Maximo.
 
©Maggid | Date:4.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 2
Hamjambo Watoto Wazuri?

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia watoto wa shule huko Moncada Garrison katika mji wa Santiago de Cuba nchini Cuba wakati wa alipotembelea nchi hiyo (Picha: John Lukuwi)
 
©Maggid | Date:4.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 1
Je, Ugumu wa Maisha Huchelewesha Kuoana?
Inasadikika kwamba ugumu wa maisha huwachelewesha vijana wa kike na kiume kuoana.

 
©Maggid | Date:4.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 11
Waheshimiwa Wakipanga Mikakati

Waheshimiwawabunge wakipanga mikakati: Kutoka kulia ni Juma Kapuya (waziri wa kazi), Rostam Aziz (Igunga), Emmanuel Nchimbi (Naibu Waziri wa Ulinzi) na Andrew Chenge (Bariadi Magharibi)
 
©Maggid | Date:4.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 1
Kila Mmoja Na Hamsini Zake!


Magogoni, DariSalama
 
©Maggid | Date:4.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Usipowakuta Wahusika....


Acha malalamiko yako chumba namba 3!
 
©Maggid | Date:4.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 1
Thursday, December 03, 2009
Blackburn na Man City Zachupa Nusu fainali Fainali Carling
Usiku wa kuamkia leo tar 3, December, 2009 timu vigogo za Arsenal na Chelsea zimetolewa katika robo fainali ya kombe la ligi(Carling Cup).
Magoli ya kipindi cha pili ya Carlos Tevez, Shaun Wright-Phillips na Vladimir Weiss yalitosha kuizamisha Arsenal kwa kufungwa magoli 3-0 na kuikweza Man City hadi nusu fainai ambazo Man City ilizikosa tangu mwaka 1981.
Magoli ya Blackburn Rovers yalipatikana kupitia kwa Nikola Kalinic na Benni McCarthy's aliyefunga kwa njia ya penati. Wakati yale ya Chelsea yalipatikana kupitia kwa Didier Drogba na Salomon Kalou.na Hivyo kulazimisha muda wa ziada kutokana na sare ya magoli 2-2. Mikwaju ya penati ndiyo iliamua mshindi kutokana na Chelsea kukosa mikwaju mitatu na Blackburn kukosa mikwaju miwili. Hivyo Blackburn wakapata tiketi ya kwenda nusu fainali kwa jumla ya magoli 4-3dhidi ya chelsea.



Golikipa wa Blackburn Rovers, Paulo Robinson aliyeibuka shujaa kwa kuokoa michomo ya penati


Wachezaji wa Manchester City wakishangilia baada ya Kuitungua Arsenal mabao 3-0 na kufanikiwa kutinga nusu fainali ya Carling Cup
 
©Maggid | Date:3.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 2
Wednesday, December 02, 2009
Ulimwengu Wa Mahaba: Je, Mwanamke Ni Katili Kitandani?


Hii ni mada endelevu. Hapa kuna hoja ya mchangiaji. Mnakaribishwa kuchangia kwa minajili ya kuelimishana.

Submitted on 2009/11/30 at 4:28am

Uzoefu wangu tofauti. Wanawake ni wakatili ajabu inapotokea akafika kileleni kabla ya mwanaume. Hawezi kuvumilia tendo liendelee kwani ....Soma zaidi; http://www.kwanzajamii.com
 
©Maggid | Date:2.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 3
Uhuru Day Ohio



The Steering Committee of the Sauti ya Wanawake wa Africa-Ohio (SWAO) has the pleasure and honor of proudly presenting the 48th anniversary of Tanzania Independence Day celebrations, in Ohio . The event will take place on Friday, December 11, 2009, at 610 Lancaster Avenue, Reynoldsburg , OH 43068 . The time-frame for the event is 7:00 PM – 1:00 AM; the event is a revival after more than 18 years when it was last celebrated in Columbus . These celebrations used to be organized by the East African Community in Columbus , OH annually during the early 80s to the early 90s.



The SWAO organization is organizing this event in the sprit of “ Tanzania volunteerism and community participation” by facilitating the pride of our heritage and patriotism for our mother nation. They hope to inspire both Tanzanians and Pan-Africans ( Tanzania enthusiasts) in Ohio to collaborate in mobilizing the community and enabling other related community events.



Kiswahili Version:

Flyer hii inahusiana na miaka 48 ya kuzaliwa kwa taifa letu pendwa la Tanzania (sikukuu ya uhuru). Mwaka huu chama cha wakina mama/dada cha SWAO (Sauti ya Wanawake wa Africa-Ohio) kimeamua kujitoa na kutayarisha shamra-shamra za sikukuu hii tukufu ya kuazimisha miaka 48 ya kuzaliwa kwa taifa letu. Hii itakua mara ya kwanza baada ya mda wa zaidi ya miaka 18 kusherehekewa kwa sikukuu hii hapa mjini Columbus , OH .



Wanachama wa SWAO wanajitolea katika kutayarisha shamra-shamra hizi, kwa nia ya kuhamasisha Watanzania wote wanaoshi Ohio na Pan-Africanist wote ambao wangependa kujiunga na watanzania katika kujivunia urithi wetu na taifa letu; na shughuli hii na zingine nyingi…ambazo wana SWAO wanategemea zita chipukiza kutokana na hamasi hii.

Akhsanteni
 
©Maggid | Date:2.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 2
Mlawa Wa MMI Steel


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MMI Steel, Aboubakary Mlawa,akiwa na pande la jiwe la chuma katika mlima wa Maganga Matitu uliopo wilayani Ludewa ambapo kampuni yake imeingia ubia na Shirika la Maendeleo la Taifa NDC kwa ajili ya kuchimba chuma ili kuzalisha bidhaa mbalimbali za chuma. ( Picha kwa hisani ya MMI Steel)
 
©Maggid | Date:2.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Haya Ndio Maganga Matitu!- Mawe Meusi


Sehemu ya mlima wa Maganga Matitu ambapo kampuni ya MMI Steel itachimba chuma kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Taifa(NDC) kupitia kampuni iliyoundwa katika ubia huo ya Maganga Matitu Resources Ltd,hivi Karibuni. ( Picha: Aboubakary Mlawa)
 
©Maggid | Date:2.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 1
Kinda Gibson Awainua Man U robo Fainali Ya Kombe la Ligi(Carling Cup)

Darron Gibson, Mfungaji wa magoli mawili ya Manchester United dhidi ya Tottenham Hospurs.
Usiku wa kuamkia leo(tarehe 2/December/2009) ulikuwa ni usiku wa chereko kwa mashabiki wa Man U pale Kinda Mu-Irish wa timu hiyo Darron Gibson alipoisaidia timu yake kuibuka na ushindi mnono wa magoli mawili dhidi ya Spurs.
 
©Maggid | Date:2.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Utambuzi:Iweje mtu asionwe wakati yupo?

Jengo la Bunge Dodoma.
KWA kawaida huwa tunajidanganya na kudhani tunajua mengi sana kuhusu maisha au yote kuhusu maisha, wakati ukweli ni kwamba tunayoyajua ni yale kidogo tu ambayo tumekutana nayo au kujifunza maishani. Mara nyingi mtu anapozungumzia nguvu fulani zilizoko kwenye dunia hii au ulimwenguni anaweza kuonekana kituko. Zaidi soma
http://www.kwanzajamii.com
 
©Maggid | Date:2.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 1
Lini Mwafrika atajikomboa kiuchumi?

Rais wa Zimbwabwe Mheshimiwa Robert Mugabe

MEI 25, 1963, mjini Addis Ababa, Viongozi wa nchi 31 za Afrika walioanzisha Umoja wa nchi huru za Afrika [OAU] siku hiyo, walikuwa na kazi ngumu kuchagua kipi kipewe kipaumbele na umoja huo, kati ya vita vya ukombozi wa kisiasa dhidi ya ukoloni mkongwe, na vita vya ukombozi dhidi ya ubeberu wa kiuchumi wa nchi za Magharibi.
Zaidi soma http://www.kwanzajamii.com
 
©Maggid | Date:2.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 5
Kuna Viongozi Mbwa Mwitu

Waziri mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine
“KUNA makundi CCM”. Hakuna makundi CCM!” “Jamani tunayaona makundi CCM” ” - CCM “Hatuyaoni makundi ndani ya CCM!” Wimbo huu tumeusikia kwa muda mrefu sasa. Kwa vile bado unaendelea kuimbwa, basi, mantiki hapa ni kuwa ‘ Kuna makundi CCM’. Maana wenye kuuimba wimbo huu ni Wana- CCM wenyewe. Zaidi soma http://www.kwanzajamii.com
 
©Maggid | Date:2.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Mvua Kubwa Jeddah


Saudi Arabia
 
©Maggid | Date:2.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Mjadala Endelevu: Digrii Ya Adam Malima


( Mjadala juu ya digrii ya Adam Malima uliibuka na kujadiliwa kwa kina mwanzoni mwa mwaka huu. Leo hii, tukiwa tukaribia mwisho wa mwaka, Bw. Nalitolela amekuja na hoja. Kwanza tutakumbushua hoja iliyoibua mjadala hapo chini na kisha tutaona ufafanuzi wa Nalitolela.

"Jamani hizi digrii za Adam Malima zinatambuliwa na Taasisi ya Elimu ya juu Tanzania?

Kufuatana na tovuti ya Bunge mheshimiwa Adamu Malima alipomaliza kidato cha nne alienda kusoma Chuo kikuu cha HAVANA CUBA digrii ya pili.Yaani kutoka kidato cha nne hadi kusoma digrii ya pili.Halafu akaenda SOAS alikosomea Postgraduate diploma na Masters degree tena.Je hizo degree zote alizonazo huyo mheshimiwa zina hadhi ya kutambuliwa na mamlaka ya Elimu Tanzania hadi kumwezesha mtu apewe unaibu uwaziri?

Kufuatana na Tovuti ya bunge

http://www.parliament.go.tz/bunge/mp_Cv3.asp?PTerm=2005-2010&fpkey=427

Elimu ya Huyo mheshimiwa ni kama ifuatavyo:

University of London (SOAS) MSc (Econ) 1994 - 1995 MASTERS DEGREE
Univesity of London (SOAS) Post Graduate Diploma (Econ) 1993 - 1994

POSTGRADUATE
University of Havana (Cuba) MSc (Economicy) 1984 -1989 MASTERS DEGREE
Shaban Robert Secondary School O-Level Education 1979 - 1982 SECONDARY
Upanga Primaru School Primary Education 1972 - 1978 PRIMARY

Hizo digrii za Cuba na hizo za SOAS zinatambuliwa hapa Tanzania?"



: Wed Dec 02, 07:26:00 AM EAT, Nalitolela, P. S.
Nilikuwa nikisaka habari fulani katika mtandao nikakutana na picha ya waheshimiwa na kusoma maoni juu hapo. Simtetei Malima wala simpingi, ila naomba niseme yafuatayo:

1. Katika baadhi ya nchi shahada ya uzamili (master's) huwa inaunganishwa na shahada ya kwanza na unasoma kwa miaka mitano, hivyo unapohitimu unapewa MA/MSc moja kwa moja. Cuba ni nchi mojawapo; pia nchi nyingi za Ulaya Mashariki ikiwamo Urusi zilikuwa zina mtindo huu na baadhi wanaendelea nao.

2. Chuo Kikuu cha Havana ni chuo kinachofahamika na kuheshimika kimataifa. Mfano kuna Professor anafundisha Ryerson University, Canada. Tovuti yake nii hapa: http://www.math.ryerson.ca/~polivares/
Huyu jamaa kasoma PhD Havana na kama ingekuwa chuo hiki hakitambuliki huyu bwana asingepata kazi Ryerson (http://www.ryerson.ca/home.html, http://en.wikipedia.org/wiki/Ryerson_University)

3. Suala la kutoka kidato cha 4 kwenda chuo kikuu sio la ajabu. Kuna mtu namfahamu alimaliza kidato cha 4 Tanzania, akaanza cha 5. Katikati ya kidato cha 5 akapata nafasi kusoma Canada katika chuo kikuwa kinachotambulika (University of New Brunswick). Katika baadhi hawana system ya A level; hata kama elimu yao ina miaka 6 ya Sekondari. Hivyo basi kwa mtu uliyehitimu kidato cha 6 Bongo inakuwa kama umesoma 1st year tayari, na unaruhusiwa kuanza masomo ya 2nd year. Hivyo basi kwa mtu aliyehitimu form 5 na kufanya vyema, anaweza kuacha kusoma A level na kuanzia 1st year. Kila nchi ina system tofauti. Cha muhimu sio umesoma kwa miaka mingapi; cha muhimu umesoma "deep" kiasi gani.

4. Ndio maana nchi kam Uingereza waliamua kufanya bachelor zao karibia zote ziwe miaka mitatu, sio kama nyumbani ambapo bado baadhi ya discipline ni miaka minne, nyingine mitatu.

5. Mara kwa mara nimeona mijadala kama hii mtandaoni. Mfano baadhi ya watu nimeshaona wakihoji mtu kutoka "Bachelors" hadi "PhD". Kwenye nchi nyingi, ikiwemo Uingereza, Marekani na Australia, kusoma Master's sio lazima na Master's kwa kawaida ni professional degree. Kwa wale wanaotaka kufanya research wanaenda PhD moja kwa moja.

6. System zipo tofauti, cha muhimu utambulike kimataifa. Mfano baadhi ya nchi Master's karibia zote ni mwaka mmoja; wakati nchi nyingine Master's ni miaka miwili.
 
©Maggid | Date:2.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 16
Riziki Hunyoshewa Mkono- Shabaan Robert

Chalinze, hivi karibuni.
 
©Maggid | Date:2.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Ofa Ya X-Mas Kwa ' Mwenyekiti!'





Juzi hapa nilipita pale Mikumi National Park nikakutana na 'ofa' ya chakula na malazi bure kwa usiku mmoja kwangu na familia yangu( Xmas eve). Ni ofa kutoka kwa Seba ( Pichani juu) Ni meneja wa hoteli. Seba ni mwenzetu pia humu ' kijijini'. Ofa hiyo ni kwa kutambua mchango wangu, si tu wa kuwapeleka wageni mahali hapo, bali pia kuitangaza mbuga hiyo ya wanyanma, vivutio na huduma zake za kitalii kupitia blogu hii. Nashukuru sana na inatia moyo.
 
©Maggid | Date:2.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 8
Tuesday, December 01, 2009
Ni Mwaka Wa Chelsea England?
Klabu ya Chelsea inayoshiriki ligi kuu ya England (Premium Liege)imeonesha mafanikio ya hali ya juu katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo. Hii imeibua maswali kadhaa miongoni mwa wadau wa soka na wengine wameshatabiri kwamba kama itaendelea na mwendo huo lazima itautwaa ubingwa wa soka nchini humo. Hadi sasa Chelsea tayari imeshinda mechi zote dhidi ya klabu kubwa za nchini humo(The Big Four)

Kocha mkuu wa klabu ya Chelse Carlo Ancheloti

Mshambuliaji hatari wa klabu ya Chelsea, Didier Drogba akifunga mojawapo ya magoli uwanjani.

Mshambuliaji hatari wa klabu ya Chelsea, Didier Drogba akishangilia mojawapo ya magoli yake msimu huu.

Wachezaji wa Chelsea wakiwa katika picha ya pamoja.

Wacheaji wa timu ya Chelsea-The blues wakiwa katika harakati mbalimbali za mafanikio ya soka.
 
©Maggid | Date:1.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 4
Waziri Mkuu Mizengo Pinda Uso kwa Uso na Lowasa

Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Atembelea Monduli..
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa wilaya na Halmashauri ya Monduli, Arusha kuhusu hali yaukame na njaa wilayani humo kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo. Kulia ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Edward Lowassa na katikati ni mkuu wilaya hiyo,Njowika Kasunga.
 
©Maggid | Date:1.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 3
Simba Taifa Kubwa
 
©Maggid | Date:1.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Unapatikana Hapa


Soko Mjinga, Kisutu.
 
©Maggid | Date:1.12.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 1
Monday, November 30, 2009
Tumekuwa Watu Wa Ovyo Ovyo!



Sanamu hiyo ya mzee anayepiga ngoma inayotoa maji ( sasa haitoi) nimeiona tangu nikiwa chini ya miaka mitano kiumri. Iko kwenye bustani ya Mnazi Mmoja wilyani Ilala. Nilipita mahali hapo jioni ya leo, pamenikumbusha utotoni. Ndio, ni enzi hizo ambapo wazazi wetu walikuja mahali hapo kupumzika nyakati za jioni na sisi watoto wao. Leo mahali hapo pamefungwa, watu wa Darisalama hawaruhusiwi kuingia hapo kujipumzisha. Muhusika hapo ameniambia wakiwaruhusu watu, basi huchafua eneo hilo hata kwa haja ndogo na kubwa! Kuna choo cha public mahali hapo, lakini ni cha kulipia.

Kwanini tunashindwa kuwa na taratibu zitakazorudisha utamaduni wa watu kujipumzisha bustanini kama ilivyo kwa jirani zetu wa Kenya pale Nairobi? Nahofia kuna watoto wa kizazi cha sasa ambao hawaelewi hata bustani ya kupumzikia ina maana gani kwao. Jamani, nahofia hata baadhi ya viongozi wakiwamo baadhi ya waheshimiwa madiwani wa jiji hawaelewi umuhimu wa bustani. Ndio, maana kuna kiroja kimetokea mjini na hakuna anayelalamika au kuandika gazetini. Pale viwanja vya Mnazi Mmoja siku hizi wanakodisha kwa ajili ya shughuli za harusi binafsi! Ndio, kwenye bustani ya umma.
Kuna wajanja wamejitengenezea kamradi kao.

Watu wa Darisalama lazima waamke na kukataa ujinga huu. Itakumbukwa miaka ya 90 enzi za Meya Kitwana Kondo kuna mfanyabiashara kwa jina la Baghdad alipewa ruhusa na jiji ajenge jengo la ghrofa la biashara katika bustani hiyo na chini kuwe na maduka yanayozunguka bustani. Basi, mfanyabiashara yule akazungushia mabati bustani ile tayari kwa ujenzi. Watu wa Darisalama walikataa ujinga ule, wakagawana mabati yale. Baadae Serikali kupitia Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi ikapiga 'stop' ujenzi huo. Walichopigania watu wa Darisalama wakati ule ilikuwa ni haki yao ya kutumia viwanja hivyo kwa mapumziko. Kinachotokea sasa hakina tofauti sana na cha miaka ile ya 90. Viwanja vya umma vilivyotengwa kama bustani ya kupumzikia kwa umma vinabinaifsishwa kiholela. Kamwe, watu wa Darisalama na Watanzania kwa ujumla hatutakubali kuchungulia kwenye matundu ya ukuta , harusi na shughuli binafsi kwenye viwanja vya umma, tena vya kupumzikia. Wahusika wabadili utaratibu huu wa sasa, wavirudishe viwanja hivi vya umma vya kupumzikia kwa wenye navyo, wananchi. Kumbi za kufanyia sherehe binafsi ziko tele mjini!
 
©Maggid | Date:30.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 11
Utalii Wa Ndani


Mikumi National Park, Jumamosi ya juzi.
 
©Maggid | Date:30.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 2
Soko Mjinga


Kisutu, leo alasiri.
 
©Maggid | Date:30.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Mtaa Wa Livingstone


Kariakoo, leo jioni.
 
©Maggid | Date:30.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Mnazi Mmoja


Leo saa kumi na mbili jioni.
 
©Maggid | Date:30.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Walikuja Kwa Mafungu, Wameondoka Kwa Mafungu !


Wageni kutoka Sweden, wameondoka jana asubuhi. Wamefurahia sana ziara yao ya juma moja.
 
©Maggid | Date:30.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
I & I !


Kigamboni, Jumapili wiki iliyopita.
 
©Maggid | Date:30.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Maelezo Mafupi


Bw. Jacob Diaz, Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo Ya Wananchi cha Anaotoglo Cha Dar es Salaam, akitoa maelezo kuhusiana na chuo hicho na shughuli zake kwa ujumbe kutoka Sweden uliotembelea chuo hicho juma la jana. Chuo hicho kinatoa mafunzo kwa vijana wenye ulemavu ikiwamo wenye mtindio wa ubongo.
 
©Maggid | Date:30.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Wanafunzi Darasani: Anaoutoglo FDC



Mnazi Mmoja Dar, juma la jana.
 
©Maggid | Date:30.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
FaceHook!

facebook t-shirts zinapatikana kwa slogan mbalimbali....wahi yako mapema!!

PRICE:15.000 TSH
COLOR: BLU, BLACK, WHITE AND GREY
SIZE: L, M,S AND FREE SIZE
LOCATION: MAYFAIR PLAZA

HIGH QUALITY

CONTACT: 0784670105 or 784670106

Cheers,

Hugo
 
©Maggid | Date:30.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 1
Uhuru Day Finland
 
©Maggid | Date:30.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Mayasa Hamad




Course :
Masters of Arts in Diplomacy, Law and
Global change
Chuo: Coventry University, United Kingdom,
Coventry
 
©Maggid | Date:30.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 6
Sunday, November 29, 2009
Utamaduni Na Utandawazi!


Somo la Profesa Mbele. Kisutu, usiku.
 
©Maggid | Date:29.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 1
Keep In Mind!
 
©Maggid | Date:29.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 3
Saturday, November 28, 2009
Nimewasili Tena Dar Salama Alasiri Hii
Nimeianza safari yangu kutoka Iringa alfajiri ya leo nikiwa na wageni kutoka Sweden. Dar ni ile ile, joto kali lakini Eid El Hajj imeifanya iwe tulivu hususan barabarani, hakuna msongamano wa magari. Nina picha kadhaa za njiani, nikipata muda nitaziingiza usiku huu au kesho alfajiri, inategemea na mtandao pia!
 
©Maggid | Date:28.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Eid El Hajj Njema!


Leo ni Eid El Hajj. Natawakia Waislamu na msio Waislamu, Eid El Hajj yenye furaha, amani na upendo.
Maggid
 
©Maggid | Date:28.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 48
Maarifa Ni Nini?


Ni kile kilichobaki katika kumbukumbu zako baada ya kusahau vyote ulivyotafuna kichwani kwako. Je, wanazuoni na msio wanazuoni maarifa kwenu ni nini?
 
©Maggid | Date:28.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 3
Heshima Mbele Kwa Mnyama Wa Taifa


Ukimgonga huyu .....
 
©Maggid | Date:28.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 4
Friday, November 27, 2009
Porini Hutakiwi Kujipeleka Mbele Mbele!



Unaweza kuwa wa kwanza kudakwa na mamba au mnyama mwingine wa hatari. Na ukiwa nyuma sana ya wenzako, unaweza kunyofolewa na mamba au mnyama mwingine wa hatari. Chunga sana pia sehemu zilizo karibu na maji wakati wa jua kali, husogelewa na wanyama wengi. Unatakiwa kuwa makini muda wote, na ndio maana ya kulipa pori heshima yake.
 
©Maggid | Date:27.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 1
Mkao Wa Kuwinda!



Jamaa si tu ana kucha kali, ana mawe pia! Simba wa Mikumi. Jumatano asubuhi tuliwaona kwa karibu wakiwa watatu na katika mkao wa kuwinda.
 
©Maggid | Date:27.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
..... Filamu Inaendelea!





Simba Wa Mikumi
 
©Maggid | Date:27.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Tafuta Tofauti!
 
©Maggid | Date:27.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 5
Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania


Kushoto ni Bw. Stellan Arvidsson wa Shirika la Misaada la nchini Sweden ( SIDA) na Bw. Reuben wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania.
 
©Maggid | Date:27.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 1
Mazungumzo Ya Kikazi


Kati ya uongozi wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania na ujumbe kutoka Chuo Kikuu Cha Linkoping. Mazungumzo hayo ya saa moja na nusu yalifanyika siku ya Jumanne ya juma hili. Pichani: Kutoka kushoto ni Profesa Bisanda, Dr. Mushi, Dr. Cornelia Muganda, Kiki, Stellan, Johan na Eva Marie.
 
©Maggid | Date:27.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
Profesa Bisanda


Deputy Vice Chancellor ( Academics) Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania
 
©Maggid | Date:27.11.09 | Permalink| | Send To Your Friend | Comment: 0
   
 
Copyright 2006 © MAGGID MJENGWA. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu